Kampuni inayoandaa video za wanamuziki mbalimbali ndani na nje ya Afrika Kusini, Godfather imekamilisha video ya wimbo wa ‘Kwetu’ wa msanii mpya, Raymond Raymond kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na msanii, Nassib Abdul (Diamond Platnumz).
Godfather amefanikisha upigaji wa picha za video hiyo nchini katika maeneo ya Tandale, Manzese na Mburahati.
Raymond kutoka lebo hiyo anakuwa wa pili baada ya Harmonize kufanya vizuri, alianza kuonyesha kipaji chake mwaka 2011 aliposhinda katika shindano la ‘Freestyle’ alipofika jijini Dar es Salaam alijumuishwa katika kundi la Tip Top Connection.
Katika wimbo huo, Raymond ameelezea namna vijana ambao ukiwatazama unaona ni watu wanaoishi maisha ya kifahari kutokana na kuwa watanashati lakini wanapokuwa katika uhusiano wanashindwa kuwapeleka wachumba zao kwao kwa kuhofia hali mbaya ya nyumbani kwao.
Post a Comment