WCB yatoa mwongozo wa adhabu wanazotoa kama msanii wao akifanya makosa
Uongozi wa label ya ‘WCB’ umesema umejipanga kikamilifu kudhibiti swala la nidhamu kwa wasanii wake.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Babu Tale amesema wao kama uongozi watasimama kidete kuhakikisha wasanii wa WCB wanakuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.
“Nikijibu hapo kwenye eneo la nidhamu ni kwamba, sisi ni vijana ambao tunaishi na vinaja ambao wametoka kwenye familia zao ambazo zinamalezi tofauti tofauti, lakini wakija hapa ni lazima wafuate sheria zetu. Sitaki kumsifia Dioamond ni mtu ambaye hana nidhamu ya kuigiza, kwa hiyo hawa wengine lazima wafuate tabia za kaka yao,” alisema Babu Tale.
Aliongeza, “Kwetu msanii akitukana kwenye social network , akitukana kwenye stage huyo lazima sisi tumuadhibu. Kuna adhabu ambayo inasukumwa na social network hiyo hatuizingatii kwa sababu kila mmoja ana mapenzi yake na wengine wanachuki zao. Adhabu ambayo tatizo linaonekana wazi kwamba hili ni tatizo, tunayaita matendo kusudi, kiofisi huwenda mtu akasimamishwa bila jamii kujua, kukata pesa kwenye kazi zake bila jamii kujua, hayo mambo tunafanyia hata sisi viongozi pale tunapokosea,”
Post a Comment