#SimbaKasema, Ngoma ya Diamond na wakali wa Nigeria, P square inatoka muda wowote kuanzia sasa.
Diamond bado hajasema jina la wimbo huo lakini tayari ameanza kuupigia promo kwenye mitandao ya kijamii, Kupitia instagram, Diamond ameandika:
“My People!!!!!!!!! Subscribe to my Youtube Channel now so that you can be the first one to watch the HIT from SIMBA ft P-SQUARE!!!! (Najua unakiu kias gani….haya Jiunge na Channel yangu ya YOUTUBE sasa ili uwe mtu wa kwanza kushuhudia Mshine yangu Mpya Nilowashirikisha P-SQUARE! ) Cc @peterpsquare @rudeboypsquare #SimbaKaseMa”
Kwa upande mwingine meneja wake, Sallam ameahidi kuwa muda ambao Subscribers wa staa huyo kwenye channel yake ya Youtube watafika laki tano video hiyo itaachiwa muda huo huo, hadi sasa wapo 287,999.
Mashabiki wa staa huyo wameonesha shauku zaidi ya kuupokea mzigo huo mpya wa Diamond Feat. P square.
Post a Comment