Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya story kubwa may 31 2016 kwenye gazeti la Habari leo yenye kichwa cha habari kisemacho” Mke wa trafiki adaiwa kukiri kumuua mumewe” gazeti hilo limeripoti kuwa mke wa trafiki wa usalama barabarani Sajent Ally ‘Kinyogori’ aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine.
Kamanda wa Police kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na police kwa mauaji hayo yaliyofanyika nyumbanii kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani
Post a Comment