Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imewatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge. Wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano wa nne.
Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wasiudhurie vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatahudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.
Post a Comment